Flavi na wenzake 4 (walifariki Nikomedia, leo Izmit nchini Uturuki, 303) ni Wakristo ambao waliuawa wakati wa dhuluma ya kaisari Diokletian kwa sababu walikataa kuabudu miungu[1].
Wanaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.